Image
Image

RAIA WA MALI WAANZA RASMI KUPIGA KURA


   Wapiga kura wakiwa wanaonekana hapo katika
Picha.


Raia wa Mali wanapiga kura leo Jumapili(28.07.2013) na kupuuzia vitisho vya waasi wa Kiislamu na kujitokeza kwa mamilioni kupiga kura kumchagua rais mpya ambaye anatarajiwa kuanzisha enzi mpya ya amani na uthabiti.

Wapiga kura watakuwa na fursa ya kuchagua miongoni mwa wagombea 27 wakati wakipiga kura kwa mara ya kwanza tangu mapinduzi ya mwaka jana katika nchi hiyo ambayo ni moja kati ya nchi za eneo hilo yenye demokrasia imara, baada ya wapiganaji wa Kiislamu walipochukua fursa ya vuguvugu la kutaka kujitenga na kudhibiti eneo kubwa la nchi hiyo upande wa kaskazini.

Uchaguzi umeanza saa nne asubuhi saa za Mali chini ya ulinzi mkali baada ya moja ya makundi ya Waislamu kaskazini ya Mali kusema jana Jumamosi (27.07.2013) kuwa litashambulia vituo vya kupigia kura.

"Vituo vya kupigia kura na maeneo mengine yatakayofanyika zoezi hilo la kupiga kura katika kile wanachoita uchaguzi yatalengwa katika mashambulizi ya Mujahideen, " kundi la vuguvugu la umoja na Jihad katika Afrika magharibi (MUJAO) limesema katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Mauritania ANI.

Taarifa hiyo haikufafanua ni njia gani zitatumika katika mashambulizi hayo.

Kundi hilo limewaonya Waislamu wa Mali kutoshiriki katika zoezi hilo la kupiga kura , likiwaamuru "kujitenga na uchaguzi huo."

Licha ya kuwa kampeni iliyochukua wiki tatu ilimalizika rasmi Ijumaa bila kutokea tukio lolote baya , hali hiyo inasababisha kutanda kwa wingu la machafuko katika eneo la kaskazini ambalo limekuwa na shaka ya kuwapo tayari kwa Mali kufanya uchaguzi ambao utakuwa huru na wa haki na wenye kuaminika.
Wakosoaji wanasema.
Wakosoaji nchini humo pamoja na nje ya nchi wamedai kuwa Mali, ikiwa chini ya mbinyo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa , inaharakisha kufanya uchaguzi huo na kuhatarisha kuwa na uchaguzi ambao hautakamilika ambao unaweza kuleta madhara zaidi badala ya hali bora.

Lakini Louis Michel, mkuu wa kundi la uangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya, ameeleza matumaini siku ya Ijumaa, akisema hali ni nzuri kwa ajili ya kufanyika duru ya kwanza ya uchaguzi wa kuaminika.

"Naamini kwamba uchaguzi huu unaweza kufanyika katika muktadha na masharti ambayo yanakubalika na hayaruhusu hali ya kutoaminika ama udanganyifu wa matokeo," amewaambia waandishi habari katika mji mkuu Bamako.
Wasi wasi mkubwa kabla ya uchaguzi huo umekuwa ukielekezwa katika mji wa Kidal, uliokuwa ukidhibitiwa kwa muda wa miezi mitano na Watuareg wanaotaka kujitenga hadi pale makubaliano ya amani yaliporuhusu jeshi la Mali mapema mwezi huu kutoa huduma za usalama katika mji huo.
Mapigano kati ya Watuareg na raia weusi wenye asili ya Afrika kabla ya uchaguzi yamesababisha vifo vya watu wanne . Na watu wenye silaha wanaofikiriwa kuwa ni kutoka la National Movement for the Liberation of Azawad MNLA wamewateka nyara maafisa watano wa tume ya uchaguzi kilometa 200 kaskazini mwa Kidal.
Uchaguzi wa kwanza.
Uchaguzi huo ni wa kwanza tangu jeshi kuasi Machi mwaka uliopita ambapo aliangushwa kutoka madarakani rais Amadou Toumani Toure ambaye alichaguliwa kidemokrasia. Mtafaruku uliofuatia ulisaidia kundi la MNLA, MUJAO na makundi mengine yenye mafungamano na al-Qaeda kulidhibiti eneo la kaskazini ya Mali.
 
Katika mkesha wa uchaguzi , kaimu rais wa Mali Dioncounda Traore, katika hotuba aliyoitoa kuptia televisheni , amewataka watu wa Mali kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi kupiga kura katika nchi hiyo ambayo watu wanaojitokeza kupiga kura kwa kawaida huwa chini ya asilimia 40. Traore binafsi si mmoja kati ya wagombea.

Kwa msaada wa Reuters.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment