Image
Image

RIPOTI INAYOONYESHA MAJIMBO YALIYO ATHIRIKA NA UKIMWI NCHINI KENYA YATOKA.



Majimbo ya Nairobi, Kisumu na Homa Bay ina mzigo mkubwa wa ugonjwa wa Ukimwi nchini Kenya.
Hii ni kulingana na uainishaji wa kwanza wa serikali wa viashiria vya kijamii katika majimbo.
Ripoti mpya iliyotolewa na Tume ya Mgawo wa Mapato inaonyesha kwamba watu 199,100 wanaishi na Ukimwi katika jimbo la Nairobi,ikiwa ni idadi kubwa zaidi katika nchi. 
Kiwango cha maambukizi kinasimama katika asilimia 8.6, juu zaidi kuliko wastani wa kitaifa, kulingana na ripoti hiyo.
Kitaifa, kiwango cha maambukizi ya VVU - uwiano wa watu wazima wenye umri miaka 15 na zaidi ambao walikuwa wameambukizwa mwaka 2011 - ilikuwa asilimia 6.2, kulingana na Ripoti ya Kenya Aids Epidemic Update 2012 iliyotolewa mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa Karatasi za ukweli wa Majimbo Kenya za mwezi Juni 2013,Nairobi ilikuwa na maambukizi mapya 13,510 mwaka 2011,ikiwa ndio ya juu zaidi kati ya majimbo yote 47 nchini Kenya.
Ripoti hiyo pia inaanika tofauti kubwa katika majimbo hasa katika umaskini, upatikanaji wa maji, umeme na viwango vya elimu Baada ya Nairobi,Karatasi za ukweli wa Majimbo Kenya zinaorodhesha Kisumu,Homa Bay,Siaya na Mombasa kama majimbo yaliyo na watu wengi wanaoishi na ukimwi.
Jimbo la Homa Bay lina watu 150,000 wanaoishi na virusi vya ukimwi,na kulifanya jimbo hilo kuwa mbebaji mkuu wa mzigo wa Ukimwi,likiwa linashikilia nambari 46.Lilikuwa na maambukizi mapya 9,500 mwaka 2011 wakati kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 27.1,mara nne zaidi ya wastani wa kitaifa.
Katika nambari 45-ya tatu kutoka chini-jimbo la Kisumu lilikuwa na watu 113,000 wanaoishi na ukimwi.Lilikuwa na kiwango cha maambukizi cha asilimia 18.7,mara tatu zaidi ya wastani wa kitaifa.Kulikuwa na maambukizi mapya 7,100 nchini Kenya mwaka 2011 pekee.
Jimbo la Siaya lina watu 100,400 wanaoishi na ugonjwa huo na lilikuwa namba 44 kati ya majimbo yote.Mwaka 2011 lilikuwa na kiwango cha maambukizi cha asilimia 17.8,ikiwa ni mara tatu zaidi ya wastani wa kitaifa.Lilikuwa na maambukizi mapya 6,300 mwaka huo.
Jimbo la Mombasa ni la tano kati ya majimbo yaliyoathirika zaidi,likiwa na watu 77,100 wanaoishi na ukimwi.Jimbo hilo liliandikisha maambukizi mapya 4,930 mwaka 2011.Lilifuatiwa na Kisii (namba 41) ambalo lina watu 73,300 wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Kulingana na Ripoti hiyo,jimbo la Wajir-lililo na watu 800 tu walio na ukimwi-lina mzigo ulio nafuu wa ukimwi.Kulikuwa na maambukizi 10 tu mwaka 2011.Kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 0.2,ikiwa ni chini zaidi ya wastani wa kitaifa.
Nalo jimbo la Lamu katika Pwani ya Kenya lilikuwa la pili kwa visa vichache vya vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi-watu 800 tu.Pia jimbo hilo liliandikisha idadi ndogo ya maambukizi mapya (10),sawa na Wajir.Jimbo la Marsabit lenye watu 1,700 walio na ukimwi lilikuwa la tatu.Lilikuwa na watu 460 ambao waliambukizwa virusi vya ukimwi mwaka 2011.
Jimbo la Mandera lilikuwa la nne.jimbo hilo lina visa 7,900 likifuatiwa na Isiolo lenye 3,200.
Takwimu kuhusiana na virusi vya ukimwi inatokana na ripoti mbalimbali za uchunguzi,tafiti na makadirio ya sensa.
Mbali na afya, ripoti hiyo pia inatoa takwimu muhimu juu ya masuala mengine ya kijamii ikiwa ni pamoja na umaskini,elimu,maji na usafi wa mazingira.
Ripoti hiyo ilisema "takwimu kuhusu maji elimu na afya, na usafi wa mazingira, upatikanaji wa umeme na barabara zote zinaelezea kukosekana kwa usawa.Tofauti hizo zinaonyesha kushindwa kwa serikali kuu kusawazisha fursa kwa wakenya wote."
Kwa mujibu wa Ripoti hiyo,Wakenya wameridhia serikali za majimbo kwa sababu wanatarajia kwamba zitasaidia kujaza mapengo ya utoaji wa huduma.
Aidha Ripoti hiyo inasema kwamba kufuatilia utendaji wa majimbo kila baada ya muda kutatoa hatua nzuri ya kiwango ambacho ahadi ya kikatiba imeweza kutimizwa.Ripoti hiyo pia imetoa wito kwa majimbo yatakayotenda vizuri yaweze kutambuliwa ili yaweze kuigwa na majimbo mengine.
Katika ripoti kama hii mwaka jana,japokuwa ilikuwa kwenye kijitabu kidogo,tume ya mgawo wa mapato ililiorodhesha jimbo la Kajiado kama jimbo tajiri zaidi wakati Turkana likiorodheshwa kama maskini zaidi.
Kenya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment