Image
Image

SERIKALI YATANGAZA MISHAHARA MIPYA KWA WATUMISHI WA UMMA, KIMA CHA CHINI NI 41.18%.


Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimuudumia mgonjwa hospitalini hapo. Wafanyakazi wa sekta ya afya ni miongoni wa walio ongezewa mishahara na serikari katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14. Picha na Maktaba. 
SERIKALI imetangaza mishahara mipya kwa watumishi wa umma itakayoanza kutumika mwezi huu, huku kima cha chini kikiongezwa kwa asilimia 41.18 kutoka Sh 170,000 hadi Sh240,000.

Vilevile, mishahara ya watumishi wengine wa umma imeongezwa kwa wastani wa asilimia 8.41. 

Waraka namba moja kwa watumishi wa umma uliotolewa na Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utum
ishi wa Umma, George Yambesi Julai 2 mwaka huu, unaeleza kuwa marekebisho hayo ya mishahara yatahusu watumishi wa serikali kuu na watumishi wa serikali za mitaa.

Wengine watakaonufaika na marekebisho hayo ni watumishi walioshikizwa kwenye taasisi za umma na watumishi ambao watakuwa kwenye likizo inayoambatana na kuacha kazi, kustaafu kazi au kumaliza mikataba baada ya Julai mosi mwaka huu.

Waraka huo umeonyesha kuwa watumishi wa serikali ambao wanapata mishahara binafsi isiyo ndani ya viwango vya mishahara ya serikali hawatahusika na marekebisho hayo.

Mei 29 mwaka huu, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, aliliambia Bunge, kwamba Serikali imekamilisha majadiliano ya kuongeza kima cha chini cha mshahara katika sekta 12 binafsi, kitakachoanza kutumika rasmi Julai mosi.

Waziri Kabaka alitaja sekta hizo kuwa ni ya Ujenzi, Shule Binafsi, Nishati, Viwanda na Biashara, Hoteli na Huduma za Majumbani, Ulinzi Binafsi, Madini, Afya, Uvuvi na Huduma za Majini, Usafirishaji, Mawasiliano na Kilimo.
 
Kwa mujibu wa Kabaka, mishahara imepanda kwa kiwango cha asilimia kati ya 21 na 65 huku Afya ikiongoza kwa kuongezwa ikifuatiwa na sekta ya hoteli na huduma za nyumbani yenye asilimia 55.

Mei mosi mwaka huu akiwa mkoani Mbeya, Rais Jakaya Kikwete, aliahidi unafuu wa maisha kwa wafanyakazi kwa kuangalia uwezekano pia wa kupunguza kodi kwenye mishahara, Lipa Kadiri Unavyopata (PAYE).

Kuhusu kuongeza mishahara, Rais Kikwete aliahidi wafanyakazi wote kwamba Serikali itaendelea kuiongeza kulingana na hali ya uchumi wa nchi. Waraka huo unaonyesha kuwa mishahara mipya kwa watumishi wa serikali kada ya masharti (operational service), ngazi ya mshahara na mshahara mpya kwenye mabano ni;

TGOS A

TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS A 3. (Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A 6. (Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A 9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A 12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh 318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A 18(Sh335,200).

TGOS B

TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B 3 . (Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B 6. (Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9. (Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11. (Sh442,000) na TGOS B 12. (Sh451,500).

MWANANCHI

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment