Image
Image

UMOJA WA MATAIFA WAIPONGEZA TANZANIA KWA KUIMARISHA UTAWALA BORA.


Hassan Abbas.



Tanzania imepongezwa na Umoja wa Afrika (AU) kwa hatua kadhaa ilizofikia katika kuimarisha utawala bora, ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa APRM, Hassan Abbas, alisema pongezi hizo zilitolewa katika wasilisho la ripoti ya nchi iliyowasilishwa na Rais Jakaya Kikwete mbele ya viongozi wenzake wa Umoja huo Januari 26, mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethopia.

“Tayari Tanzania tumeshakamilisha zoezi hili la kwanza la aina yake na uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo utafanyika Oktoba, mwaka huu na serikali imepewa muda wa kufanyiakazi maeneo yenye changamoto,” alisema.

Alisema tayari serikali imeonyesha dhamira ya dhati kwa kuanza utekelezaji wa maoni mbalimbali ya wananchi kama vile kuendelea kusimamia utekelezaji na kuripoti kwa umma na baada ya uzinduzi wa ripoti, masuala mengine kuingizwa katika mipango na bajeti za miaka ijayo za wizara na taasisi nyingine husika.

Baadhi ya masuala yaliyobainishwa na ambayo yanahusu katiba yaliwasilishwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na mengi yameingizwa kwenye rasimu iliyotolewa hivi karibuni pamoja na mengine kuingizwa kwenye mfumo wa mpango wa mwaka na bajeti ya serikali iliyopitishwa hivi karibuni.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment