Image
Image

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YAKE MPYA YA HAKATWI MTU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM.


 Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na Meneja masoko Airtel money Rwebu Mutahaba wakionyesha Bango la hakatwi mtu wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini.






Kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania Airtel  imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha inayojulikana kama ‘Hakatwi mtu hapa’ yenye lengo la kuwawezesha  wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa kupitia huduma hiyo bila makato yoyote.





Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini, Kushoto Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa (kulia) Meneja masoko Airtel money Rwebu Mutahaba.






Hata hivyo promosheni hiyo  itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.






Kauli hiyo imetolewa muda mfupi na wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo na  Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando ambapo  alisema

 “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa kuzindua promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya kifedha nchi nzima”.






Kwa upande wa Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.





“Tunayofuraha kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo hapo awali. 
Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa akiongea na wahandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure itakayo wawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure, pichani Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando.





Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.




Airtel kwa sasa inaendesha promosheni maalumu kwa wateja wake ya Airtel yatosha. 

Promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’ ni msisitizo unaoonyesha Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote nchini. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment