Image
Image

MWENYEKITI WA CUF IBRAHIM LIPUMBA AMTAKA RAIS KIKWETE NA IGP MWEMA KUANGALIA KWA JICHO LA TOFAUTI MATUKIO HAYA YA KUHATARISHA AMANI YA NCHI YANAO TOKEA KILA UCHAO HUSUSANI KUTILIA MKAZO LA KUPIGWA RISASI SHEKH PONDA.


                             Prof. Ibrahim Lipumba

Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na taasisi za kiislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda anayedaiwa kupigwa risasi na polisi mkoani morogoro mara baada ya kumalizika mhadhara aliokuwa akihutubia, amelazwa chini ya uangalizi katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Taarifa za kulazwa kwa kiongozi huyo zimetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye alikwenda kumjulia hali hii leo.
                          Sheikh Ponda Issa Ponda
Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  mara baada ya kumtembelea katika wodi ya dharura katika hospitali ya taifa ya Muhimbili amesema tukio hilo ni miongoni mwa matukio mabaya yanayodaiwa kufanywa na vyombo vya dola ambayo hayana budi kudhibitiwa kwani yanaweza kuwa na madhara kwa ustawi wa taifa. 

"Cama cha Cuf kinasikitishwa sana na kufadhaishwa na Mwendelezo wa vitendo vya kikatili vya mauaji ya raia yanayo fanywa na jeshi la polisi kwa kisingizio cha kulinda amani ya nchi, huu utaratibu au sera ya piga tu tumechoka itatufikisha pabaya alisema Lipumba.
Aidha Prof. Lipumba  Amemwomba Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini inspekta Jenerali Saidi Mwema kuhakikisha kuwa matukio ya kupigwa risasi wananchi wasiokuwa na silaha yanakomeshwa lakini pia wanaohusika kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria.

                           Rais Jakaya Kikwete
Hata hivyo Prof.Lipumba amevitahadharisha vyombo vya dola hususan jeshi la polisi kuhakikisha kuwa linaondoa vizingiti vya kupatiwa matibabu sheikh Ponda ,ambapo pia amewataka waislam pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa na subira wakati sheikh ponda akiendelea kupatiwa matibabu.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment