Image
Image

UKARABATI WA MIUNDO MBINU WA MAJI SAFI KATIKA MAKAZI YA ASKARI POLISI MBIONI KUKAMILIKA.



Semvua Musangi.
Ofisi ya Mbunge wa Ilala kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TRA wanakamilisha ukarabati wa mfumo wa miundombinu ya maji safi katika makazi ya askari Polisi wa kituo cha Msimbazi kilichopo Kariakoo jijini Dar es Salaam, ili kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa maji kwenye makazi hayo yaliyopo kwenye jengo la gorofa.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kariakoo kuangalia maendeleo ya Mradi huo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama hicho kata ya kariakoo Halima Abdallah amesema mradi huo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Halima Abdallah Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama.

Amesema mkandarasi anayefanya kazi hiyo atahakikisha maji ya bomba ambayo kwa sasa yanapatikana chini pekee yatapandishwa hadi kwenye gorofa hizo, ili kila wakazi waliopo kwenye gorofa husika wanapata huduma hiyo walipo badala ya kulazimika kushuka hadi chini kuteka maji.

Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo Filbert Luhanyula amesema anaamini mradi huo utaleta nafuu kwa familia za askari wanaoishi kwenye jengo hilo ambao kwa sasa wanapata usumbufu wa kupandisha maji juu kwa kutumia ndoo na madumu.
Filbert Luhanyula Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo

Kondo Thabit - Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa - Kariakoo Kaskazini.

Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni nane na laki nane, utanufaisha Jumla ya familia themanini za askari polisi wanaoishi kwenye jengo hilo la gorofa nne.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment