Image
Image

SERIKALI YA TANZANIA YAKABIDHIWA BILIONI 1001 NA JUMUIYA YA ULAYA IKIWA NI MSAADA WA KIBAJETI



Jumuiya ya Ulaya imekabidhi kiasi cha Shilingi Bilioni 101 kwa Serikali ya Tanzania, ikiwa ni msaada wa Kibajeti kwa ajili ya kuimarisha zaidi maeneo muhimu kwenye malengo ya Millenia MDG.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa amesema fedha hizo zinalenga kuiongezea uwezo Serikali ya Tanzania katika kupunguza umasikini, ili kufikia malengo ya Maendeleo ya Millenia.

Mwaka 2009 Serikali ya Tanzania ilisaini makubaliano na Jumuiya ya Ulaya ambapo EU itatoa Euro Milioni 305 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 654.7 kwa serikali ya Tanzania ili kuiwezesha kutekeleza maeneo muhimu kwenye Malengo ya Maendeleo ya Millenia kwa kipindi cha miaka sita.

Kwa upande wake, Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini Filberto Sebregondi amesema Umoja wa Ulaya umeridhika na hatua chanya zinazochukuliwa na Tanzania kuelekea malengo ya Maendeleo ya Millenia.

Misaada ya Jumuiya ya Ulaya na washirika wengine wa kimaendeleo, imeisaidia kwa kiasi kikubwa serikali ya Tanzania kupambana na umasikini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment