Image
Image

UTOUH:MCHAKATO WA UKAGUZI UNAHUSU RASILIMALI ZA UMMA KUONGEZA UWAZI NA UWAJIBIKAJI.


                                        UTOUH

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovic Utouh amesisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa umma katika mchakato wa ukaguzi mbalimbali unaohusu rasilimali za umma ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika matumizi na udhibiti wa rasilimali za taifa hususan fedha za umma.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika semina kwa watendaji mbalimbali wakiwemo wabunge, watendaji wa halmashauri, wakaguzi wa ndani na nje ya nchi pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia,Bwana Uttoh, amesema suala la uwazi na uwajibikaji katika ngazi ya jamii halipaswi kuachwa kwa taasisi za ukaguzi pekee, bali linapaswa kushirikisha jamii kupitia asasi zisizo za kiserikali pamoja na vyombo vya habari.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu huyo wa hesabu za serikali amesema semina hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na ofisi ya taifa ya ukaguzi (NAOT), imelenga kujenga uwezo wa namna ambavyo wanaweza kushirikisha umma katika ukaguzi na kufikia katika mapendekezo ya namna wananchi ambao ndio wahusika wakuu watashirikishwa katika zoezi hilo muhimu na kupata njia tofauti za kushirikisha umma.

Nao washiriki wa semina hiyo wamesema ushirikishwaji uliokuwepo ni wananchi kupatiwa taarifa kwa kubandikiwa katika mbao za matangazo kwenye halmashauri za wilaya, hali ambayo haikuwa ya ushirikishwaji kikamilifu na kwamba wanamatumaini semina hiyo itasaidia kubaini njia muafaka za ushirikishwaji wa umma.

Wakaguzi kutoka nje ya nchi wanaoshiriki semina hiyo ni pamoja na kutoka Ufilipino, India pamoja na Argentina.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment