Shahidi wa tano
katika kesi ya kutorosha wanafunzi inayomkabili Mchungaji wa Kanisa la TAG,
raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Jean Felix Bamana ameieleza
mahakama namna alivyolazimishwa kufanya mapenzi na mchungaji huyo.
Shahidi huyo,
Angela Swai (19), akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu, Naomi Mwerinde wa
Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, alisema Mchungaji huyo alimlazimisha kufanya
kitendo hicho jaribio ambalo lilishindikana kutokana na mshitakiwa huyo kukataa
kutumia kondomu.
Akiongozwa na
mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Esther Majaliwa, katika ushahidi wake,
Shahidi huyo alieleza Mahakama hiyo alivyokutana na mshtakiwa kwa mara ya
kwanza na mara ya pili ambapo alisema alikutana naye kupitia marehemu mama yake
mzazi huku mara ya pili akikutana naye kupitia mtandao wa kijami.
Shahidi huyo
alieleza mahakamani hapo kuwa alikutana na mshtakiwa kwa mara ya kwanza kupitia
mama yake na alimtambulisha yeye na mdogo wake aliyemtaja kwa jina la Arthur
kuwa mchungaji huyo ni baba yao mwingine na waliendelea kufahamiana kwani alikuwa
ni rafiki mkubwa wa mama na mshirika wake katika Biashara ya Madini.
Alisema kwa
kipindi kirefu hakuwahi kumuona hadi alipokutana naye kwa mara ya pili mwaka
jana kupitia mtandao wa Facebook ambapo alimwomba urafiki kwa nia njema kwani
alikuwa ni rafiki mkubwa wa marehemu mama yake, na kuongeza kuwa mawasiliano
yalikuwa ni ya kawaida tu.
Shahidi huyo
alisema baada ya hapo mshtakiwa alianza kumsisitiza kuhamia Dar es Salaam kwa
ahadi ya kumsaidia kuendelea na masomo baada ya kumueleza amefukuzwa shule
jambo ambalo yeye binafsi alilikataa.
Alisema baada
ya kukataa kukubaliana na wazo la kwenda Dar es Salaam, mshtakiwa huyo
alimwambia atafika Moshi ambapo alifikia katika Hoteli ya Moshi View, Februari
14, mwaka huu na kufanya naye mawasiliano kupitia simu ya mdogo wake aliyetajwa
mahakamani hapo kwa jina la Arthur Swai, akimtaka kumfuata hotelini hapo
0 comments:
Post a Comment