Image
Image

VIONGOZI CCM WAFUNGIWA MLANGO TAWI LA SINZA DAR ES SALAAM, KUTOKANA NA KUSADIKIWA KUWEPO KWA HARUFU YA RUSHWA KATIKA OFISI HIYO.


 Mlango wa Katibu wa  CCM wa tawi la Sinza E ukiwa umepigiliwa mbao kwa misumari kuzuia uongozi kuingia ndani.



 Mlango wa Katibu wa  CCM wa tawi la Sinza E ukiwa umepigiliwa mbao kwa misumari kuzuia uongozi kuingia ndani.
 Sehemu ya kulaza magari inayolalamikiwa na vijana wa CCM tawini hapo.
 Vijana wa CCM wakilinda geti ili viongozi wasiingie ofisini.…

 VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Sinza E jijini Dar es Salaam wamefungiwa milango na vijana wa chama hicho kwa madai kuwa kuna ubadhirifu wa fedha katika ofisi hiyo.

Mwenyekiti wa Vijana  wa Tawi hilo, Ally Ngoti ameuambia mtandao huu kuwa tangu viongozi wao waingie madarakani wamekuwa hawaelezi mapato ya ofisi hiyo yanakwenda wapi.

“Hapa tuna miradi mingi kama vile egesho la magari ambalo linaingiza mamilioni ya fedha lakini hatuoni zinakwenda wapi. Kuna fremu za maduka na watu wamepanga lakini fedha hatuzioni, tumeamua kufunga milango ya ofisi ili wasiiingine mpaka kieleweke,” alisema Ngoti na kudai kuwa viongozi hao hawawapendi vijana kwa kuwa wanawakosoa.

Hakuna kiongozi hata mmoja aliyepatikana kujibu tuhuma hizo au kusema watafanya nini ili kufungua ofisi yao.

(PICHA / HABARI: HARUNI SANCHAWA / GPL)
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment