Image
Image

SHEIN APANGUA BARAZA LA MAWAZIRI ZANZIBAR NA KUUNDA WIZARA MPYA.


                    Dk. Ali Mohamed Shein.

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kupangua idara zilizokuwa zikisimamiwa na wizara mbalimbali na kuunda wizara mpya nne.



Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, katika mabadiliko hayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kubakia na Wizara 16 kama ilivyokuwa zamani.



Taarifa hiyo imetaja Wizara mpya zilizoanzishwa ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Idara maalum za SMZ ambayo Waziri wake atakuwa Haji Omar Kheir, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora itakayoongozwa na Dk. Mwinyihaji Makame.



Wizara nyingine ni Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, itakayoongozwa na Haroun Ali Suleiman na Wizara ya Fedha ambayo itakuwa chini ya Omar Yusuph Mzee.

Katika mabadiliko hayo idara zilizohamishwa kutoka Wizara moja kwenda nyingine ni idara ya uwezeshaji ambayo imehamishiwa katika Wizara ya Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto ambayo itaongozwa na Waziri Zainab Omar Mohamed.

Idara nyingine ni utumishi wa umma na utawala bora na kuhamishiwa katika ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, shughuli za tume ya mipango zimehamishiwa ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi kutoka Wizara ya Fedha na idara ya uratibu wa shughuli za SMZ Dar es Salaam zimehamishiwa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.



Aidha, Dk. Shein amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu wakuu katika Wizara hizo mpya na mabadiliko hayo ameyafanya kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment