Image
Image

CHINA NA AFRIKA ZATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUPATA MAENDELEA KWA PAMOJA.



Mazungumzo ya tatu ya kisiasa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa China na nchi za Afrika yamefanyika jana alasiri katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. 
 Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, China na Afrika zinatakiwa kushirikiana ili kupatia maendeleo kwa pamoja. 

Mawaziri hao wamebadilishana maoni kuhusu ushirikiano kati ya pande hizo mbili, pia wamepitisha taarifa ya pamoja ya mazungumzo ya tatu ya kisiasa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa China na Afrika. 

Bw. Wang Yi amesema, kutimia kwa ndoto ya China kunategemea jitihada za wachina, pia kunahitaji uelewa na uungaji mkono kutoka kwa watu wa nchi mbalimbali duniani. 

Amesisitiza kuwa waafrika wapatao bilioni 1 wanafanya juhudi ili kutimiza ndoto ya Afrika ya ustawi na maendeleo. 

Bw. Wang amesema, China na Afrika ni za jumuia ya mustakabali wa pamoja, na zinategemeana sana katika njia ya kupata maendeleo. 
Anasema,"Siku zote China ni rafiki wa dhati na mwaminifu wa Afrika, tutaimarisha ushirikiano kati yetu na marafiki zetu barani Afrika ili kupatia maendeleo kwa pamoja. 

Tutawanufaisha wananchi wetu, lakini pia tutatoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kutimiza amani ya muda mrefu na ustawi kwa pamoja."

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment