Image
Image

MCT YASEMA VYUO VIWILI TU VYA UANDISHI WA HABARI NCHINI NDIVYO



Baraza la habari Tanzania MCT limesema ni vyuo viwili tu vya uandishi wa habari nchini vilivyokidhi vigezo vya kutumia mitaala  ya kisasa yenye ithibati ya baraza la Taifa la Elimu ya ufundi NACTE,inayolenga kutilia maanani uwezo wa mwanafunzi kwenda kufanya kazi inayotarajiwa.

Akitoa taarifa mbele ya waandishi  wa habari kufuatia matokeo ya ukaguzi wa pamoja wa hivi karibuni baina ya MCT na NACTE,katibu mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga,amesema,lengo la ukaguzi huo lilikuwa kubaini uwezo wa vyuo hivyo  ngazi ya cheti na Diploma katika kutumia mitaala hiyo kwa kuangalia vigezo vya vifaa,taaluma,Pedagogia,Miundombinu na uongozi.

Bwana Mukajanga,amevitaja vyuo hivyo kuwa ni cha A3 Institute of Professional Studies  cha Dar Es Salaam na cha Arusha Journalism Training cha Arusha.

Amesema vyuo vitano vimepewa hadi Desemba mwaka huu kukamilisha vigezo vinavyotakiwa kufundishia mitaala hiyo yenye lengo la kuongeza weledi katika taaluma ya habari inayotoa nafasi kubwa ya kazi za vitendo kwa wanafunzi.

Katika hatua nyingine,meneja wa udhibiti na viwango wa MCT, Pili Mtambalike amewatoa wasiwasi,wale wote wenye vyeti vya zamani  kuwa mazungumzo yanaendelea kati ya MCT na NACTE,ili kuvitambua  kuvifanyia ulinganisho na kuvitambua vyeti hivyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment