Mahakama ya New Delhi, India imetoa hukumu ya kifo kwa
wananume 4 waliombaka mwanamke mmoja na kisha kumuua Disemba mwaka uliopita.
Jaji Yogesh Khanna akitoa hukumu hiyo amesema dhulma dhidi ya wanawake
zimeshtadi mno katika miaka ya hivi karibuni nchini India na kwamba adhabu ya
kifo inatolewa kwa washtakiwa ili iwe funzo kwa watu wengine wenye tabia kama
hiyo.
Wanaume hao wanadaiwa kumbaka kwa zamu mwanamke mmoja
kwenye basi na kisha kumtesa hadi kufa. Mshukiwa mwingine wa kesi hiyo
alipatikana amejitia kitanzi gerezani. Kesi hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa zaidi
ya miezi saba na kufuatiliwa kwa karibu na vyombo vingi vya habari vya
kimataifa.
Uchunguzi unaonyesha kuwa visa vya ubakaji na dhulma
dhidi ya wanawake ni jambo la kawaida nchini India kutokana na utamaduni wao
unaomsawiri mwanamke kama chombo tu cha kupambia dunia.


0 comments:
Post a Comment