Makundi ya wanawake nchini Zimbabwe yamekasirishwa na uamuzi
wa Rais Robert Mugabe wa kuteuwa wanawake watatu pekee katika baraza lake
la mawaziri 2.
Akitetea uamuzi wake, Rais Mugabe amesema ni sharti wanawake
wafanye vyema zaidi katika chaguzi ili waweze kupewa viti vya uwaziri.
Wanawake
nchini humo wanasema usawa wa kijinsia upo mbali sana kufikiwa.
Inaelezwa kuwa ni asilimia 12
tu ya wanawake kwenye baraza la mawaziri ikilinganishwa na idadi ya wanawake
nchini humo ambayo ni asilimia 52 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi
iliyofanywa mwaka jana.
Baada ya kuwaapisha mawaziri Jumanne iliyopita, Rais Robert
Mugabe aliwaambia waandishi habari kuwa, hakuna la kustaajabisha kwamba
wanawake ni wachache kwenye baraza hilo.
Alisema wanawake wanapaswa kupambana
na wenzao wa kiume bila kutegemea kupendelewa kwa namna yoyote.
Katiba mpya ya Zimbabwe iliyoidhinishwa mapema mwaka huu
inaelezea vipengele vya kisheria vinavyolinda wanawake ikiwemo kuwa na
haki sawa katika ajira na uwakilishi sawa katika ofisi zote za umma,
ambapo inategemewa kwamba usawa huo ni pamoja na uwakilishi
kwenye baraza la mawaziri.
Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa
Afrika SADC ambayo Zimbabwe ni mwanachama ina sheria inayosema wanawake wawe na
uwakilishi wa kisiasa kwa asili mia 50 ifikapo mwaka wa 2015.



0 comments:
Post a Comment