Image
Image

WAZIRI MKUU WA SOMALIA AAHIDI KULITOKOMEZA KUNDI LA AL SHABAB.




Waziri Mkuu wa Somalia ameahidi kuliangamiza kundi la kigaidi la al Shabab lililofanya mashambulizi na kuua watu wengi katika jengo la maduka la Westgate mjini Nairobi, Kenya.

 Abdi Farah Shirdon Saaid amesema wanajeshi zaidi ya elfu 17 wa vikosi vya AMISOM wapo Somalia na kwamba ana imani kuwa Mogadishu itafanikiwa kuliangamiza kundi la al Shabab kwa kusaidiwa na  wananchi na jamii ya kimataifa.

Waziri Mkuu wa Somalia amesema Somalia na Kenya zitaendeleza mapambano dhidi ya kundi la al Shabab na kwamba Mogadishu haitasalimu amri mbele ya matakwa ya kundi hilo kwamba wanajeshi wa Kenya wanapaswa kuondoka katika ardhi ya Somalia. 

Kundi la al Shabab limetangaza kuhusika na shambulio hilo la Westgate huku likisema kuwa limefanya hivyo kulipiza kisasi kwa hatua ya Kenya ya kutuma wanajeshi wake huko Somalia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment