Image
Image

BAADA YA KUFANIKISHA ZOEZI LA KUWAKABILI AL SHABAB KENYATA ATANGAZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA NCHINI HUMO.


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kumalizika kwa mzingiro wa jengo la maduka la Westgate huko Nairobi baada ya wafanya mashambulizi sita kuuliwa na 11 wengine kutiwa nguvuni na vikosi vya usalama vya nchi hiyo. 

Kenyatta amesema mapambano makali ya kuwakomboa mateka na kuwanasa wafanya mashambulizi huko Westgate yamemalizika na kwamba vikosi vya usalama vya Kenya vimetoa pigo na kuwafedhehesha wafanya mashambulizi hao.

Amesema raia 61 na wanajeshi sita wameuliwa katika mkasa huo wa Westgate.

Aidha  Rais Kenyatta ametangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia leo Jumatano.   
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment