Mzee wa
kusugua benchi: Nahodha wa Arsenal,Vermaelen amepoteza nafasi ya kuanza kikosi
cha kwanza klabuni kwake
Anapambana
katika klabu yake na timu yake ya Taifa ya Ubelgiji ili kulinda nafasi yake.
Vermaelen
amepoteza nafasi hiyo na kumuacha kocha wake, Arsene Wenger kuwatumia zaidi
Laurent Koscielny na Per Mertesacker.
Hata katika
kikosis cha Ubelgiji bado ana kazi kubwa ya kugombania nafasi na wachezaji
wakali ambao ni Vincent Kompany na Jan Vertonghen.
Majukumu ya
kimataifa: Vermaelen akiwasili katika mazoezi ya Ubellgiji sambamba na nyota wa
Tottenham, Jan Vertonghen
Benched:
Vermaelen (top left) sits alongside Nicklas Bendtner and Nacho Monreal with
Jack Wilshere in front at the Emirates.
Wanasugua
benchi: Vermaelen (mstari wa nyuma kushoto) akiwa amekaa benchi na Nicklas
Bendtner na Nacho Monreal, huku naye Jack Wilshere mstari wa mbele akiwa
anasugua katika dimba la Emirates.
Kwa msaada
wa Sportsmail
...........................................................................................................
Na Ismael Mohamed (Bin majid)
BEKI wa
washika bunduki wa kaskazini mwa London, klabu ya Arsenal, Thomas Vermaelen
amekiri kuwa ataanza kufikiria hatima yake ya baadaye klabuni hapo kama
atashindwa kuingia kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger.
Beki huyo wa
kati aliyeanza katika kikosi cha timu yake ya Taifa ya Ubelgiji dhidi ya Wales
mjini Brussels jumanne ya leo alisema ataanza kuangalia kwa umakini maamuzi
yake ya kubaki au kuondoka kama ataendelea kuanzia benchi Emirates, kwani siku
zote mchezaji mwenye kipaji kama yeye hapaswi kuwa nje ya kikosi cha kwanza.
Kikosi cha
Ubelgiji kilifuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za kombe la dunia mwakani
baada ya ukame wa miaka 12 siku ya ujumaa ya wiki iliyopita baada ya kushinda
mbele ya Croatia.
Safari hiyo
ya Brazil tayari imeingia kichwani mwa beki huyo wa kati na sasa anafikiria
nafasi yake ya kucheza kikosi cha kwanza cha timu yake ya Asernal ili
kumshawishi kocha mkuu wa timu ya Taifa yake ya Taifa, Marc Wilmots kumfikiria katika safari hiyo ya
mafanikio.
Alipoulizwa
nafasi yake Emirates, Vermaelen alisema: ‘Natakiwa kuliwaza hilo pale
itakapobidi. Imebaki miezi michache kufikia januari. kiukweli, kutocheza kamwe
hakutanisaidia katika safari yangu ya kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani
Brazil”.
“Watu
wananiuliza kama sichanganyikiwi wakati huu ambao sichezi sana, lakini haiko
hivyo”.




0 comments:
Post a Comment