Image
Image

HIVI USHAA KAA NA KUFIKIRIA KWAMBA DOKII HUENDA ANGEWEZA KUZUNGUMZA NENO LA AJABU KWA WALE WATU WANAO FUATILIA MAISHA YAKEE, NA KUSEMA KWAMBA WOTE NI..........



Nyota wa sinema za Kibongo, Ummy Wenceslaus maarufu kama  'Dokii' amewashangaa watu wanaomsema kuwa anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete na kuwataka waache propaganda zisizo na tija  kwani yeye hajipendekezi hata kidogo. 

Amelazimika kutoa kauli hiyo wakati wa mahojiano yake na Kipindi cha Action & Cut kinachorushwa na kituo  cha Channel Ten hivi karibuni, ambapo Dokii alisema kutokana na jinsi alivyoshiriki katika kampeni mbalimbali za Kikwete hadi kupata ajali na kuumia mkono, wambeya wamekuwa wakimzushia kuwa alijipendekeza na hakupewa msaada wowote alipoumia jambo ambalo sio zuri.

“Nawashangaa wanaosema kuwa najipendekeza kwa JK, eti wanasema nilitelekezwa. Kwa taarifa yao tu ni kwamba, JK aliposikia nimepata ajali, alituma madaktari Wazungu kuja kunihudumia.
 
“Halafu hata wakisema najipendekeza pia naweza nikakubali, nisipojipendekeza kwake wanataka nikajipendekeze  kwa nani? Najua hata wao wanatamani kuwa karibu na viongozi kama mimi,” alisema Dokii.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment