Image
Image

MAALIM SEIFU AWATAKA WAZANZIBARI KUISHI KWA UPENDO NA AMANI BILA CHOKOCHOKO.



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi kuacha tofauti zao na badala yake waishi kwa kuvumiliana.


Maalim Seif ametoa kauli hiyo jana wakati akitoa mkono wa Iddi el-Hajj kwa baadhi ya wazee na mayatima wa vijiji vya Jumbi, Chwaka na Marumbi katika Wilaya ya Kati Unguja.

Amesema hakuna haja kwa wanajamii kuendeleza migogoro isiyokuwa ya lazima, kwani haina tija yoyote kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyengine Makamu wa Kwanza wa Rais amewasisitiza wananchi kusherehekea sikuu ya Eid-el-Hajj kwa njia za amani na kufuata maadili ya Kiislamu pamoja na maadili ya Zanzibar.

Mapema asubuhi Maalim Seif alijumuika na viongozi wengine wa kitaifa pamoja na waislamu mbali mbali katika sala ya Eid iliyosaliwa kitaifa katika viwanja vya Marumbi na baadaye kujuika katika Baraza la Eid-El-Hajj lililofanyika Chuo Kikuu Cha Taifa cha Zanzibar kilichoko Tunguu.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment