DAR
ES SALAAM/IRINGA.
RAIS Jakaya Kikwete amesema maadui wote ambao walitaka
kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kwa lengo la kuvuruga amani ya nchi
wamedhibitiwa .
Rais
Kikwete alisema kuwa Serikali yake itaendelea kulinda amani ya nchi na maadui
wote wanaohusika na kutaka kuvuruga nchi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Kulikuwapo na upepo mbaya, lakini kwa sasa Tanzania ni shwari na tumemshinda
adui,” alisema Rais Kikwete jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya
Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yaliyoandamana na sherehe za
kuzima Mwenge wa Uhuru, mkoani Iringa.
Alisema
katika siku za hivi karibuni, maadui wasioitakia mema Tanzania walikuwa na
mkakati wa kuvuruga amani ya nchi, lakini Serikali kwa kushirikiana na vyombo
vya dola vimewadhibiti na nchi iko salama.
Rais
Kikwete alisema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa amani
kwa sababu inajua wazi kwamba nchi ikiingia kwenye mgawanyiko, mshikamano
utavurugika na shughuli za maendeleo zitasimama.
Katiba
Mpya.
Rais
Kikwete alisema mwaka 2014 ni mwaka wa kipekee kwa nchi kwa kuwa utakuwa na
mambo makubwa matatu yatakayofanywa.
Rais
Kikwete alisisitiza kwamba Katiba Mpya ni lazima ikamilike mwakani kama mambo
yatakwenda kama ilivyopangwa.
Vilevile,
alisema mwakani Tanzania itasherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyoondoa udhalimu na kuwarudishia Wazanzibari heshima ya mwanadamu na utu
wake.
“Pia
tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wetu. Nawaomba Watanzania wajiandae
kuyafanikisha vizuri mambo hayo ili historia mpya ifunguliwe nchini.
“Wazanzibari
waanze miaka mingine baada ya miaka hamsini ya uhuru wao, muungano uanze miaka
mingine baada ya miaka hamsini na Katiba Mpya itupeleke miaka mingine tukiwa
wamoja,” alisema Kikwete.
Rais
Kikwete alionya kuwa asingependa mchakato wa kupata Katiba Mpya uligawe taifa
na kuleta mfarakano utakaovunja umoja wa kitaifa badala ya kuuimarisha.
“Tunataka
tuwe na Katiba itakayojenga, siyo kubomoa, kutugawa kwa misingi ya kiitikadi,”
alionya Rais Kikwete.
Source/ mluguru.com


0 comments:
Post a Comment