Image
Image

Ligi kuu ya Zanzibar Grand Malt - Chuoni 1 KMKM - 0


MAAFANDE wa KMKM juzi walishindwa kutamba mbele ya Chuoni kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar Grand Malt uliochezwa Mao Tse Tung mjini Unguja.

Mchezo huo ambao ni mwendelezo wa ligi Kuu ya Zanzibar ulikuwa na ushindani kiasi huku miamba hiyoikienda mapumziko wakiwa hakuna aliyeweza kuuona mlango wa mwenziwe.

Katika mchezo huo ambao ulichezeshwa na mwamuzo Mfaume Ali timu ya Chuoni iliweza kujipatia bao hilo kupitia kwa mchezaji wake Amour Bakari katika dakika ya 50 ya mchezo huo.

KMKM ambayo ni kipigo cha pili tokea kuanza kwa ligi hiyo ambapo kipigo cha kwanza walikipata kwa timu ya Malindi kwa kufungwa kwa idadi kama hiyo ya bao 1-0 huku ikilazimishwa sare mara mbili na Timu ya Polisi na KMKM.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho uwanjani hapo kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Mtende Rangers ambao ndio vinara wa ligi hiyo wenye pointi 16 na timu ya Miembeni.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment