Image
Image

WACHUNGUZI WA MAMBO NCHINI KENYA WAGUNDUA MABAKI YA MIILI YA WATU KWENYE JENGO LA WESTGATE.


Wachunguzi wa Kenya wanaoendelea na uchunguzi katika jengo la Westgate lililokumbwa na tukio la kigaidi wamegundua sehemu za miili ya watu na bunduki tatu aina ya AK 47. 

Ofisa mmoja anayeshiriki kwenye uchunguzi huo amesema wamepata fuvu la mmoja wa watu wanaoamini kuwa ni magaidi wanne waliouawa kwenye operesheni ya uokoaji. 
Amesema bado kuna miili na sehemu za miili ya watu kwenye kifusi cha jengo hilo.
Mwanzoni mwa mwezi huu wachunguzi waligundua gari iliyotumiwa na magaidi kwenda kufanya shambulizi, na hivi karibuni wamegundua vitu vingi vinavyosaidia katika uchunguzi. 

Mpaka sasa watu 40 wamekamatwa na wanahojiwa na kuhusiana na tukio hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment