Hawa Ghasia - Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa.
Waziri wa
nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia
amesema ukosefu wa elimu ya nidhamu ya
matumizi ya fedha kwa wastaafu nchini
kunachangia kwa kiasi kikubwa kuwa na maisha duni mara baada ya kulipwa mafao
yao kwa mkupuo.
Akifungua
mkutano wa 6 wa mwaka wa wadau wa mfuko wa pensheni wa LAPF waziri ghasia
amesema waajiri wengi nchini bado hawajawa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa
wastaafu watarajiwa pale muda unapofika hali ambayo imekuwa ikichangia
kushindwa kutumia vyema mafao yao.
Kwa upande
wake waziri wa kazi na ajira Gaudensia Kabaka amesema mifuko ya hifadhi ya
jamii na waajiri nchini bado wanakazi kubwa ya kuelimisha jamii umuhimu wa
kuchangia kwenye mifuko hiyo ili waondokane
na dhana kuwa mifuko hiyo ni
kwajili ya watumishi wa serikali na watu matajiri tu.
Mkutano huo
wa siku mbili unawashirikisha wadau mbalimbali wa mfuko huo zaidi ya mia tano
kutoka ndani na nje ya nchi ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa na kaulimbiu ya
mkutano huo mwaka huu ni kukidhi kwa mafao ya kustaafu changamoto na njia za
kuboresha.
0 comments:
Post a Comment