Baadhi ya wanafunzi shule ya jkt wakionekana wakisikiliza jambo kwa umakini mkubwa juu ya siku ya maadhimisho ya mtoto wa kike (Picha na Maktaba Yetu).
Serikali imesema bado inaangalia uwezekano wa
kuweka utaratibu wa kumrudisha shuleni mtoto wa kike aliyekatisha masomo baada
ya kupata ujauzito.
Hatua hiyo
inafuatiwa kubainika kwamba idadi kubwa ya watoto wa kike wanaopata ujauzito
hawafanyi hivyo kwa kupenda bali kwa kulazimishwa ama kurubuniwa na wanaume
wakatili .
Hali hiyo
imebainishwa na Mkurugenzi wa masuala Mtambuka katika Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Dk. Leticia Sayi wakati akizungumza katika maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo
amewataka wadau wa masuala mbalimbali wakiwemo wa elimu kuungana na serikali
kuhakikisha vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya mtoto wa kike vinakomeshwa
kwani vimekuwa na athari kubwa kimwili, kisaikolojia na kiuchumi.
Baadhi ya wasichana wakiwa wanajadiliana jambo(Picha na Maktaba Yetu).
Maadhimisho
ya siku ya kimataifa ta Mtoto wa Kike kwa Tanzania yameratibiwa na Shirika la
Wanawake katika Sheria na Maendeleo WILDAF Tawi la Tanzania kwa kushirikiana na
Mtandao wa Wanawake Waelimishaji Afrika FAWE yakiwa na kauli mbiu ya Ubunifu kwa
ajili ya Elimu ya Wasichana.
0 comments:
Post a Comment