Hii Ndio meli yenye urefu wa Mita 250 ikionekana ikiwa
imebeba makontena Baada ya kutia nanga hii leo katika Gati la Bandari ya Dar es
Salaam.
Na. Salum Mkambala,DSM.
Tanzania kwa
mara ya kwanza imepokea meli kubwa yenye urefu wa mita 250 sawa na uwanja wa
mpira wa miguu miwili na nusu ambayo inauwezo wa kubeba kontena elfu nne na mia
tano zenye futi ishirini elfu ikiwa ni siku moja tu tangu serikali irudishe
utaratibu wa awali kwa kipindi cha mwezi mmoja wa kupitisha malori katika
mizani hapa nchini.
Hii Ndio meli yenye urefu wa Mita 250 ikionekana ikiwa imebeba makontena Baada ya kutia nanga hii leo katika Gati la Bandari ya Dar es Salaam, Huku baadhi ya watu wakiitizama kwa ukaribu kufuatia ukubwa iliyo nao.
Akishuhudia
meli hiyo iliyopewa jina la MAERSK CUBANGO ikitia nanga katika gati ya bandari
ya DSM waziri wa uchukuzi Dkt,HARRISON MWAKYEMBE ameeleza kuwa Tanzania
haijawahi kupokea meli kubwa kama hiyo na mara nyingi meli tulizozea ni za
kubeba kontena 2000 tu na meli kama hizo huwa zinaishia katika Bandari ya
Mombasa nchini Kenya.
Aidha
Dkt,MWAKYEMBE ametumia nafasi hiyo kuwatolea wito taasisi za mabenki na TRA
pamoja zingine mtambuka katika shuguli za kupakua na kupakia mizigo
bandarini kukesha katika bandari ili
kupunguza mizigo katika bandari hiyo ambapo amesema kwa sasa katika kipindi cha
muda kadhaa bandari hiyo itakuwa ikifanya kazi kwa saa 24.
Waziri wa Uchukuzi nchini DK. Harrison Mwakyembe, Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa meli hiyo yenye urefu wa Mita 250, ambayo inaonekana ikiwa imebeba makontena Baada ya kutia nanga katika Gati la Bandari ya Dar es Salaam, Huku baadhi ya watu wakionekana kumsikiliza waziri huyo akizungumza kwa umakini.
Hii Ndio meli yenye urefu wa Mita 250 ikionekana ikiwa imebeba makontena Baada ya kutia nanga hii leo katika Gati la Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza
mbele ya waziri huyo kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari
NCHINI,TPA.mhandisi,MADENI KIPANDE ameeleza mgomo wa siku nne wa wamiliki wa
malori umeiletea hasara ya sh.bilion 1.5 bandari hiyo ambapo meli 18 zilikwama
nje ya bandari na meli tisa zilikwama katika GATI ya bandari ambapo meli hiyo
imeletwa kwa majaribio kwa ushirikiano wa wakala wa meli ya MAERSK na mamlaka
hiyo baada ya kufanya utafiti wa kina ambapo nahodha mtanzania Abdul Mwingamno
alifanikiwa vyema kuegesha meli hiyo katika gati.
Wakati huo huo wakiwawakilisha wafanyabiashara wenzao wa malori mfanyabiashara AZIM DEWJI na KARIM LADHA wamedai licha ya serikali kumaliza mgomo kusubiri kamati kutoa majawabu lakini magari yanazuiwa kupita katika mizani ambapo wanatarajia kuifikisha wizara ya ujenzi mahakamani baada ya kufanya tathmini ya hasara waliyoipata.
Haya ni malori yakiwa yanaonekana na nyuma yakionekana makontena.
0 comments:
Post a Comment