Image
Image

UMAARUFU WA MAREHEMU NYAISANGA WAWALIZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA.


Pichani kati ni Marehemu, Julius Nyaisangah akiwa na wadau enzi za uhai wake, pichani kulia ni Othman Michuzi na Kushoto ni Abhoubakar Lyongo.


Mtangazaji na mwandishi wa habari wa siku nyingi nchini Tanzania  Julius Nyaisanga Maarufu kama Anko JJ amefariki dunia Jana asubuhi katika Hospitali ya Mazimbu Mkoani Morogoro.

Nyaisanga Ambaye alikuwa Meneja wa Abood Media Amekuwa Akisumbuliwa na shinikizo la Damu pamoja na Kisukari jambo ambalo limepelekea hadi kufikwa na Umauti.

Mapema Baadhi ya waandishi wa Habari wa mkoa wa Morogoro ambao wakikuwa wamefanya kazi na Marehemu na wengine wanao Mfahamu, walisema kuwa Nyaisanga ameacha pengo kubwa sana Ktika tasnia hii ya Habari kwani alikuwa mtu wa watu, huku wengine wakisema kuwa Hawatamsahau na umahiri wake wa kutangaza habari na kufanya vipindi kwemye radio.

Walisema wakati nyaisanga yupo RTD wanamkumbuka na kipindi chake cha PB ambacho alikuwa akikitendea haki, huku Radio one Wakimkumbuka kama Babu wa Kimanzichana, sambamba na mambo mengine mengi.

Marehemu Nyaisanga Alishawahi kufanya kazi Radio Tanzania Wakati huo ikiitwa RTD, Sambamba na kwenye makampuni ya Ipp Media ikiwamo ITV/Radio One.

Marehemu amefariki Dunia Akiwa Na Umri wa miaka 53, na Ameacha mjane na watoto watatu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment