Image
Image

ABSALOM KIBANDA APEWA TUZO YA UANDISHI WA KISHUJAA NA ULIOTUKUKA NA UTUMISHI YA DAUDI MWANGOSI JIJINI MWANZA.





Mjane  wa Daudi  Mwangosi Itika  Mwangosi kulia  akifuatilia matukio  yanayoendelea  katika ukumbi  huo.

Mhariri wa magazeti ya New Habari (2006)Ltd Bw. Absalom Kibanda watatu kutoka kushoto waliokaa mstari wa mbele aki bofya kifaa chake katika Tuzo hizo. 


Na Mwandishi Wetu.
Waandishi wa Habari nchini  wametakiwa  kujenga  umoja katika  kupinga sheria  kandamizi  ya  vyombo  vya habari  na  wanahabari nchini inayatarajia  kupitishwa na  wabunge wa  bunge la jamhuri ya  muungano wa Tanzania.

Meneja  wa uthibiti  wa ubora  kutoka  baraza la habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike ametoa  kauli hiyo  leo  jijini Mwanza wakati  wa hafla  ya  kukabidhi tuzo  ya  kishujaa na uandishi  uliotukuka  ya  Daudi Mwangosi .

Mtambalike  amesema  kuwa  idadi ya  waandishi  kutekwa na kuuwawa  imezidi  kuongezeka  hapa nchini  huku kasi  ya  serikali  kuvifungia vyombo  vya habari  pia  inaendelea  kuongezeka .

Hivyo iwapo wanahabari  nchini  hawataungana  katika  kupinga  manyanyaso  dhidi  ya  vyombo vya habari na  kupinga  sheria  kandamizi  dhidi ya  vyombo  vya habari na wanahabari suala  la uhuru  wa  vyombo  vya habari nchini  litaendelea  kubaki ndoto.

Kwa  upande wake rais  wa umoja  wa  vilabu  vya  waandishi  wa habari Tanzania  (UTPC) Keneth Simbaya alisema  kuwa tuzo  hiyo  inayotolewa ni  tuzo ya  kwanza  kutolewa nchini Tanzania  kwa  waandishi  wanaopata  matatizo wakati  wanatekeleza wajibu  wao.

Simbaya  alisema kuwa UTPC  imeamua  kuanzisha  tuzo  hiyo kama  njia ya  kuwapa  moyo  wanahabari na  kuuthibitishia umma kuwa  wanahabari  nchini  hawatakata tama katika  kutumikia tasnia  hiyo.

Alisema iwapo  jamii inapaswa  kujua ni vema  serikali  kukubali  kutoa habari kwa jamii inayopasa  kujua na  inayo haki ya  kupata  habari.

“ Serikali itambue  kuwa  inapohitaji  wananchi  kuchangia maendeleo ni vema itambue  kuwa  wananchi hao  wana haki ya kupata  taarifa  mbali mbali  ya kile  walichochangia….ndani  ya  tukio la mauwaji  ya  Mwangosi tumejifunza mambo mengi sana kwani tunapofanya kazi  zetu  wapo  wasiopenda  kuona  tunafanya kazi  zetu hiyo”

Pia  alisema  ni vizuri wananchi  kutambua  kuwa wakati  wanahabari nchini  wakitetea  kupata  habari wasifikiri  wanahabari  wanajipangani  wao  .

Kwani  alisema  kuwa  jitihada za  wanahabari  kupigania  uhuru  wa kupata  habari zinapaswa  kuungwa mkono na kila raia  wa Tanzania  ambayo ana haki ya  kupata  habari.

Jaji mkuu wa  tuzo  hiyo Hamza Kasongo alisema  kuwa mchakato  wa kumpata  mshindi  ulifanyika kwa kipindi  cha miezi miwili kuanza septemba hadi Octoba mwaka  huu.

Tuzo   hiyo ya  uandishi  wa  habari wa  kishujaa na utumishi  uliotukuka  ya Daudi Mwangosi  imetolewa kwa  Absalom Kibanda mhariri  wa kampuni ya  New habari (2006) Ltd  na mwenyekiti  wa  jukwaa la  wahariri nchini (TEF).

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment