Image
Image

HARAMBEE KKKT USHARIKA WA KIJITO NYAMA LOWASSA AHIMIZA UBORESHAJI ELIMU UWE KWA VITENDO.


                               Edward Lowassa.

Dar Es Salaam.
Licha jitihada kubwa zinayofanywa na serikali kwaajili ya  kuhakikisha kuwa na  ongezeko la shule na vyuo, bado zipo changamoto kubwa zinazolikabili taifa ya  namna ya kuhakikisha ubora wa elimu inayotolewa kwenye shule na vyuo hivyo inaweza kumkomboa wananchi na kumwezesha kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Waziri mkuu mstaafu ambe pia ni mbunge wa Monduli Edward Lowassa  Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangia mfuko wa elimu na ujenzi wa shule ya awali inayotarajiwa kujengwa na kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama, kwa shilingi millioni mia mbili hamsini zikiwa gharama za awali.

Amesema wakati nchi ipo katika mjadala wa namna ya kuboresha elimu nchini, inatia moyo kuona wengine wameamua kutekeleza mjadala huo kwa vitendo na kuongeza kuwa ukombozi wa kweli wa mtanzania utapatikana pale tu uhakika wa kupata elimu bora utakapofanikiwa.

Kupitia mfuko wa elimu wa usharika wa Kijitonyama matarajio ni kujenga shule ya awali katika eneo hilo la kanisa, pamoja na kujenga shule ya msingi na sekondari ambapo eneo limepatikana maeneo ya Maguepande Kinondoni jijijni dar es salaam.
Katika harambee hiyo jumla ya shilingi millioni 615 zimepatikana ambapo Bwana Lowassa na rafiki zake wamechangia jumla ya shilingi millioni sitini.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment