Image
Image

ZAIDI YA WATU MILIONI TATU NA HAMSINI HUUGUA UGONJWA WA KISUKARI, NA IFIKAPO MWAKA 2030 ZAIDI YA WATU 530 DUNIANI KUUGUA UGONJWA HUO RIPOTI YABAINI.



Tatizo la ugonjwa wa kisukari nchini (Diabetes) linaongezeka kwa kasi kubwa ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2000 asilimia sita ya watu mijini waligundulika kuwa na ugonjwa huo hali ambayo inahitaji mikakati ya kukabiliana nao.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti ulifanyika nchini miaka ya themanini, wagonjwa wa kisukari nchini kote vijijini na mijini walikuwa ni asilimia moja, ambapo utafiti wa mwaka 2000 ulionyesha idadi hiyo kufikia asilimia 6 mijini  na asilimia 1.6 vijijini. 

Aidha takwimu zinaonyesha kuwa hivi sasa, zaidi ya watu millioni mia tatu na hamsini duniani kote wana ugonjwa wa kisukari na inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2030,  watu million 530 duniani watakuwa na ugonjwa huo.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha magonjwa ya kisukari na moyo cha St Laurent Dk Mary Mayige wakati wa kliniki ya wazi, na bure ya kupima kisukari wakazi wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.

Dk Mayinge ametaja baadhi ya sababu zinazochangia watu kupatwa na ugonjwa wa kisukari kuwa ni pamoja na kutokula vyakula vya asili, mfumo mzima wa maisha wanaoishi watu hivi sasa, pamoja na watu wengi kukosa uwiano kati ya urefu na uzito wao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment