Image
Image

TANZANI YAUNGANA NA NCHI NYINGNE DUNIANI KUOMBOLEZA KIFO CHA BABA WA TAIFA WA AFRIKA KUSINI NELSON MADELA



Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuomboleza kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela aliyefariki dunia jana nyumbani kwake mjini Johannesburg baada ya kuugua ugonjwa utokanao na maambukizi ya mapafu.

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Grashia Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo hicho cha Mzee Mandela.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya rais Ikulu, rais Kikwete ameuelezea msiba wa Mzee Mandela kama msiba wa Afrika kwa ujumla hasa kutokana na mchango uliotolewa na kiongozi huyo katika harakati za ukombozi na kuongeza kwamba Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.

Rais Kikwete amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, ambapo katika kipindi hicho bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

anchi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment