Image
Image

WAKULIMA KUWEKEWA BIMA KATIKA KILIMO ILI KUEPIKANA NA HASARA ITOKANAYO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI



Mapinduzi katika sekta ya kilimo yataweza kufanikiwa endapo wakulima kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu watawekewa bima katika kilimo chao itakayowasidia kuepuka hasara inayosababishwa hasa na mabadiliko ya tabia nchi.

Ushauri huo umetolewa jijini DSM na kamishna wa bima nchini, ISRAEL KAMUZORA wakati Wa hafla ya kuanza ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya kimataifa ya bima UAP na ya hapa nchini CENTURY, utakaowezesha wakulima wa ukanda wa afrika mashariki kufaidika na huduma ya bima hatua itakayosaidia kukuza sekta hiyo ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa.

Awali akizungumzia ubia huo wa utoaji huduma za bima katika ukanda wa nchi za afrika mashariki,mkurugenzi mkuu wa UAP GROUP na mkurugenzi mkazi wa UAP CENTURY wamedai kampuni hiyo kwa sasa imeanza na uwekezaji wa bilioni 9 na tayari ina matawi 12 katika ukanda huo ambapo sekta ya kilimo,madini na maswala ya anga na nyinginezo zitaweza kufaidika katika nchi hizo.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment