Image
Image

Abiria 100 wa Air Tanzania Wakwama.


Air Tanzania
Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya Air Tanzania wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari za shirika hilo la ndege kuarishwa. 
 Wengi wa abiria hao walikua wakifanya safari kuelekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, wakielekea Mtwara na Kigoma, wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.
kutokana na kadhia hiyo shirika hilo lililazimika kukodi hoteli kuwahifadhi abiria hao kama ilivyo ada inapotokea dharura wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka lini

Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro.
Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment