Image
Image

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam yamuachilia huru Lukaza



                                        Mwesigwa Lukaza 



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachilia huru
Mwenyekiti  wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesiga lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika  akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona Hana hatia  katika Kesi iliyokuwa ikimkabili.
Hukumu hiyo Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.
Lukazambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa  akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.


                                          Johnson Lukaza
Akisoma hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama  imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo mbalimbali, Mahakama yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru  washitakiwa wote Wawili kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta  ushahidi thabiti ambao ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia  washitakiwa Hao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment