Image
Image

Breaking News:Kiongozi wa wafanya Biashara Afikishwa Mahakamani,Prof.Lipumba Hali mbaya akimbizwa Hospitali,Mbatia alipuka.


                                         Morogoro Wagoma.

Na kwa taarifa ambazo tunazo hadi sasa ingawa migomo inaendelea baadhi ya mikoa Morogoro napo yaelezwa kuwa wafanya biashara wamegoma kufungua maduka yao

Kinara wa Mgomo wa Wafanya biashara apandishwa kizimbani Dodoma Muda huu.

Kiongozi wa wafanya biashara Bwana Johnson Minja aliyekamatwa na jeshi la Polisi  jana tayari leo tarehe 28 amefikishwa katika  Mahakama kuu kanda ya Dodoma akikabiliwa na makosa mawili,1.kosa la uchochezi,2.Kuhamasisha wafanya biashara kukataa matumizi ya mashine za kieletronic za kutokla risiti za EFDs.

Hata hivyo inaelezwa kuwa baada ya kufikishwa mahakamani hapo kutokana na makosa ya awali aliyoelezwa ila taratibu za dhamana zinafanyika ilikuweza kuachiliwa.Fuatana nasi katika habari zetu tutakujuza kwa kila hatua.

          Katika Siasa: Lipumba hali mbaya,Mbatia alipuka Bungeni.

Mwenyekiti wa CUF Prof.Lipumba Amekamatwa tena na jeshi la polisi baada ya kuachiwa muda mfupi uliopita wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo imeelezwa kuwa hali yake sinzuri na kakimbizwa hospitali baada ya Presha kupanda Gafla.

Prof.Hali yake imebadilika ghafla wakati akiwa katika mahakama kuu ya Kisutu Jijini Dar es Salaam na hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya UN kinondoni DSM.

Hata hivyo leo hii bunge  lilishindwa kuendelea na shughuli zake za Bunge kwa mujibu wa utaratibu na ratiba ya Bunge hilo na kulazimika kuahirisha shughuli zake za bunge baada ya wabunge wa upinzani kusimama na kupiga kelele kwa kutaka hoja ya Mh.James Mbatia ya kutaka bunge liahirishe shughuli zake za kawaida za bunge kwa nia ya kujadili kitendo cha Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahimu Lipumba pamoja na viongozi waandamizi wa chama hicho kupigwa na Polisi jana.

Baada ya Mh.Mbatia kuwasilisha hoja hiyo Spika wa bunge alitaka serikali kutoa tamko kesho ili kutoa fursa kwa wabunge kulijadili jambo hilo lililokataliwa na wabunge wa upinzani wakitaka jambo liwezekanalo leo lifanyike leo ndipo hali ya hewa bungeni na kelele nyingi za kutoelewana kutokea na kulazimu Spika makinda Kuahirisha Bunge Hadi Jioni. 




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment