Image
Image

Breaking News:Mwenyekiti wa CUF alamba kipigo kutoka kwa askari wakati wa maandamano akiwa na wafuasi wa chama hicho temeke jijini Dar es Salaam Muda huu.




Jeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa  chama cha wananchi CUF  waliokuwa wakiandamana  kwa ajili ya kukumbuka  ya mauaji  ya wenzao waliofariki  huko Pemba Mwaka 2001.Kwenye maandamano hayo alikuwepo mwenyekiti wake Profesa Ibrahimu Lipumba  ambapo inaarifiwa kwa amepata kipigo na kuumia sehemu mbali mbali huku waandishi wa habari wakikutana na kadhia hiyo hali ambayo imewafanya wafanye kazi zao kwenye mazingira magumu.Maandamano hayo ambayo yalikuwa na wafuasi wa CUF yamefanyika Mtoni kwa azizi alli Temeke jijini Dar Es Salaam ambapo wameshindwa kuendelea na maandamano hayo kutokana na nguvu kubwa iliyotumika eneo hilo huku watu wakikimbia ovyio ovyio ili kujinusuru ingawa inaelezwa wapo walio pata majera mbali mbali.Chanzo cha sakata hili hadi kuzuiliwa na kupigwa na mabomu ya machozi.

Profesa Lipumba alikamatwa Dar es Salaam  wakati akiongoza maandamano yaliyoanza ofisi za chama hicho wilayani Temeke kwenda kwenye viwanja vya Zakhiem, Mbagala ulikopangwa kufanyika mkutano huo wa hadhara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyokuwa imetolewa na chama hicho, maandamano hayo ilikuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuomboleza vifo vya wana-CUF na wananchi wengine zaidi ya 70 waliouawa Zanzibar Januari 27, 2001, wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya urais Zanzibar.

Chama hicho kilisema siku ya jana ilikuwa ni sehemu ya kukumbuka mateso waliyofanyiwa wana-CUF waliondamana Tanzania Bara likiwemo tukio la kuvunjwa mkono kwa Profesa Lipumba, wakati wa maandamano hayo. Pia bendera zote za CUF siku ya jana zilipepea nusu mlingoti.

Wakati Polisi wakiwa wametoa amri ya kuzuia maandamano hayo kutokana na kuwa na viashiria hatari, kulitokea malumbano baina ya wafuasi wa CUF na Polisi.

Malumbano hayo yalianza baina ya maofisa wa CUF na Polisi, kabla ya Profesa Lipumba kuwasili katika Ofisi ndogo za Chama hicho zilizopo wilayani Temeke, ambapo polisi walikuwa wametanda kuhakikisha maandamano hayo hayafanyiki.

Baada ya kuwasili Profesa Lipumba, malumbano pia yaliendelea na pande zote kuonekana kutofikia mwafaka, lakini baadaye pande hizo zilikubaliana maandamano yasifanyike badala yake waende viwanja vya Zakhiem kwa magari yao.

Wakiwa kwenye magari baada ya kufika Mtoni Mtongani, msafara wa Profesa lipumba uliokuwa ukiongozwa na Polisi ulikutana na kundi kubwa la wapenzi na wanachama waliokuwa wamejipanga kumpokea kwa maandamano.

Hali hiyo iliwalazimu Polisi kuanza kufyatua mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya wafuasi hao, huku Profesa Lipumba akishushwa kwa nguvu kwenye gari alilokuwa amepanda na kuingizwa kwenye gari la polisi kitemi, huku akionekana akilalamika kutokana na msukosuko aliokuwa anapata wakati akiingizwa kwenye gari hilo.

Baada ya kuingizwa kwenye gari hilo, liliondoka kwa mwendo wa kasi na kuacha wafuasi wake wameduwaa. Kamanda wa Operesheni Maalumu Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Saimon Sirro, alikiri kukamatwa kwa Profesa Lipumba na kwamba taarifa kamili zitatolewa baadaye.

"Ni kweli Mwenyekiti Lipumba tunamshikilia lakini kwa sasa ni mapema kutoa taarifa, hivyo subiri hadi baadaye tutatoa taarifa rasmi," alisema Kamanda Sirro.

Mkurugenzi wa mipango na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Sheweji Mketo, alisema kuwa Chama hicho kiliomba kibali cha kufanya maandamano hayo ambayo wanafanya kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka Watanzania ambao wengi wao walipoteza maisha katika vurugu za kisiasa Zanzibar na wengine kukimbilia nchi jirani.

Alisema walishangazwa na kauli ya jeshi hilo ya kuzuia maandamano hayo wakati wao walitoa taarifa ndani ya saa 48 kama utaratibu unavyo elekeza.

"Chama cha Wananchi (CUF) tuna utaratibu wa kila mwaka kwa mwezi na tarehe kama ya jana kuadhimisha kumbukumbu ya watu waliokufa katika vurugu za kisiasa za mwaka 2001; hivyo lazima tufanye maandamano," alisema Sirro.

Alisema kuwa, Jeshi hilo lilipaswa kutoa taarifa mapema kama wao walivyopeleka maombi ya kufanya maandamano, lakini wamesubiri bado siku moja, tena jioni; huku saa za kazi zimekwisha ndio walipeleka majibu ya kuzuia maandamano.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment