Image
Image

Edgar Lungu ashinda Urais Zambia




Waziri wa Ulinzi na Sheria wa Zambia Bwana  EDGAR LUNGU  ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais wan chi hiyo katika uchaguzi uliofanyika mapema juma hili.

Ikitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo imesema Bwana LUNGU ameshinda kwa asilimia  48.3 .

Aliyekuwa mpinzani wake mkubwa Bwana  HAKAINDE HICHILEMA  wa chama cha  United Party for National Development, amepata asilimia  46.7  ya kura zilizopigwa.

Uchaguzi huo uliitishwa baada ya kifo cha aliyekuwa rais wan chi hiyo  MICHAEL SATA  Oktoba mwaka 2014.

Bwana LUNGU anayetarajiwa kuapishwa leo amesema amevitaja baadhi ya vipaumbele vya serikali atakayoinda kuwa ni kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na rais aliyemtangulia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment