Image
Image

Wananchi Mkoani Manyara waitaka kamati ya Bunge kuunda tume kuchunguza Miradi ya maji ukiwemo wa Vijiji 10





Wananchi wa vijiji viwili vya loto na seloto wilayani babati mkoani manyara wameitaka kamati ya kudumu ya bunge,kilimo, mifugo na maji kuunda tume ya kuchunguza miradi ya maji ukiwemo ule wa visima miradi ya vijiji 10 inayofadhiliwa na benki ya dunia katika halmashauri ya wilaya ya babati kwa kuwa imeonyesha kuuwepo kwa usiri na kujengwa chini ya  kiwango,sanjari na hilo wakiilalamikia kuundiwa bodi ya maji kwa nguvu ambayo imekuwa haitoi taarifa za mapato na matumizi kwa miaka mitatu sasa.


Malalamiko hayo wameyatoa kwa kamati hiyo iliyofika kata ya dareda katika ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya maji na kuangalia thamani ya fedha kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa(THE BIG RESULT NOW) na hapo ndipo wananchi hao walipotupia lawama  halmshauri hiyo  kuwaunganisha miradi mitatu ya maji ya water,aid,mradi wa kanisa katoliki-(DMDD)na ule wa benki ya dunia kuwepo katika mtandao mmoja,aidha kutokushirikishwa na kuhoji miradi ya wafadhili huku pia wakitishia kuacha  kulipa maji kwa mfumo wa mita na kuikataa bodi iliyopo.

Hata hivyo mkurugenzi wa maji mijini kutoka wizara ya maji BI MARY MBOWE akitolea ufafanuzi wa mgogoro huo uliopo kati ya wananchi hao na halmashauri hasa pale walipomtaka mkurugenzi huyo kutambua kuwa watalipia maji hayo endapo kamati zao zitasimamia miradi hiyo.

Akitoa msimamo wa kamati ya kudumu ya Bunge ya maji kilimo na mifugo,mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la babati vijijini BW JITU VRAJILAL SONI ameiagiza ofisi ya katibu tawala mkoani manyara kwa kushirikiana  uongozi wa bonde la kati utoa elimu ya uundwaji wa vyombo vya maji na juu ya usimamizi wa raslimali maji ili kuondoa mgogoro huo wa muda mrefu.

Kamati hiyo ya kudumu ya bunge imefanya ziara katika vijiji hivyo viwili vya loto na seloto kufuatia miezi michache iliyopita wananchi wa vijiji hivyo waliandamana kupinga kunyimwa taarifa za mapato na matumizi ya miradi hiyo ya maji,aidha pia wakilalamikia hofu iliyopo ya matumizi makubwa ya fedha katika mradi wa  visima unaofadhiliwa na benki ya Dunia.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment