Image
Image

Kufuatia TFDA kupiga marufuku uingizwaji wa Dawa zisizo na ubora nchini wafamasia wasema Wamechelewa.




Siku chache  baada ya mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kufuta usajili wa Dawa aina tano na kuzuia uingizaji,uuzaji na matumizi yake , wafamasia  wauzaji   wamesema hatua hiyo imechelewa na kuitaka mamla hiyo kuweka mikakati thabiti ya kufanikisha zoezi hilo ambalo linalenga kunusuru maisha na afya za watanzania.


Wamesema wamekuwa wakilalamikia Dawa hizo na kutoa ushauri kwa kipindi kirefu huku wakieleza wasiwasi wa baadhi ya wauza Dawa kutokuwa waaminifu na kuendelea kuzizungusha sokoni kama wanavyofanya kwa Dawa zilizokwisha muda wake.

Kwa upande wa wamiliki wa maduka ya Dawa nchini pamoja na kueleza TFDA kuwashirikisha kikamilifu kabla ya kutangaza rasmi hatua hiyo wameitaka pia kuwekeza katika matangazo kwa vyombo vya habari na mabango na kuchukua hatua stahiki kwa watao kaidi amri hiyo kutokana na kubainika kuwa na athatri mbaya zaidi kwa afya na maisha ya Binadamu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment