Image
Image

Uteuzi wa mawaziri na manaibu aliofanya Rais Jakaya Kikwete wapokelewa kwa hisia Tofauti




Mabadiliko ya Baraza la mawaziri alilofanya Rais Jakaya Kikwete  viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na Dini pamoja na  wananchi wa kawaida wametoa maoni yao huku wengine wakipongeza huku  mwenyekiti wa taifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema mhe Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa ukawa  akisema hakuna jambo jipya kwa sababu  bado sura ni zile zile.

Mh.Mbowe amesema hakuna jambo jipya katika baraza hilo kutokana na ukweli  kuwa  watu  ni wale wale ila amebadilishwa wizara  na hivyo ni sawa na kwamba hakijafanyika  chochote.

Kwa upande wake mwenyekiti wa taifa wa jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi CCM  Mh. Abdalah Bulembo amesema  mabadiliko aliyoyafanya Rais  ni yenye tija  na kuongeza kuwa kitendo cha Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu ni ishara ya kukubali matokeo ili kukinusuru chama cha mapinduzi.

Naye Sheikh Rajabu Katimba ambaye ni  msemaji wa jumuiya ya taasisi za kislamu  amesema kujiuzulu Prof muhongo  na kuteua baraza lingine siyo  Dawa peke bali  waliokula fedha za umma wawajibishwe.

Kwa upande wawananchi  Bi.Mary Massawe na Bw .Peter  Karia wamewataka viongozi waliobaki madarakani kutambua kuwa wamepewa jukumu kubwa na wajifunze kutoka kwa wenzao kwani taifa linawategemea na siyo kufanya mambo kama vile nchi haina.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment