Image
Image

Anne Kilango awaagiza Wakuu washule za sekondari kushirikiana na walimu wapya katika wanaopangiwa katika vituo vyao vya kazi

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ANNE KILANGO MALECELA amewaagiza wakuu wa shule za sekondari nchini kushirikiana na walimu wapya wanaopangiwa katika shule zao ili waalimu hao wasiondoke katika vituo vyao vya kazi.
Naibu Waziri huyo wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ametoa kauli hiyo mkoani PWANI wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu kwa wakuu wa shule za sekondari nchini za serikali na zisizo za serikali mafunzo ya kuwajengea uwezo wa juu uongozi na ufanisi katika shule wanaozoziongoza.
Naibu waziri huyo amewataka wakuu hao waangalie namna wanavyoweza kufanya kazi na waalimu wapya wanaotoka vyuoni ili kuwafanya walimu hao wapende kazi yao na wasitoroke katika vituo vyao vya kazi kwa visingizio vya ugumnu wa mazingira.
Mapema akimkaribisha naibu waziri huyo, mtendaji mkuu wa wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu nchini Dokta SISON MASANJA amesema mafunzo hayo kwa wakuu wa shule za sekondari zote nchini yanalenga kuwajengea uwezo juu ya uongozi na usimamizi fanisi wa shule zao.
Kwa upande wao wakuu hao wamekiri kupata changamoto kubwa pindi wanapopokea waalimu wapya jambo ambalo wakati mwingine wanalazimika kuwachukulia hatua za kuwawajibisha bila hata kuwashauri.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment