Image
Image

Serikali yaombwa kuwanyanganya leseni waganga wajadi wasio waadilifu nchini

Katibu wa Chama cha Watu wenye ulemavu wa Ngozi – ALBINO mkoani MBEYA - WILLIAM SIMWALI amesema kuwa vitendo vya upigaji RAMLI mkoani humo vitamalizika endapo serikali itawanyang’anya leseni waganga wa tiba asilia wasio waadilifu.
SIMWALI ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya serikali mkoani MBEYA kwa kushirikiana na wananchi kuanza zoezi la kuwabaini watu wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya upigaji RAMLI mkoani humo.
Kwa mujibu wa takwimu za waganga wa tiba za asili mkoani Mbeya wanafikia waganga zaidi ya 3,000 mkoa mzima, ambao wengine wanadaiwa kwenda kinyume na kanuni na sheria za kazi zao.
Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya ndiyo inayohusika na kutoa vibali vya waganga wa Tiba ya asili kupitia sheria Namba 23 ya mwaka 2002 ya Tiba ya asili nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment