Image
Image

Breaking News:Mbunge wa mbinga John Komba afariki dunia katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.


Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Mbunge wa mbinga magharibi Kapteni John Komba amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho katibu wa Uenezi wa  CCM Nape Nnauye amesema Mh.Komba amefariki na mwili wake tayari umehamishwa kutoka Hospitali ya TMJ na sasa umehifadhiwa hospitali ya Jeshi Lugalo.
Mpaka kufa kwake Kapteni John Komba alikuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmasauri Kuu ya CCM Taifa na Kiongozi wa bendi ya TOT.
"Bwana alitoa, Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe"


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment