Image
Image

FIFA kumchunguza Diafra Sakho mshambuliaji wa timu ya taifa Senrgal




Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka duniani FIFA inachunguza ni kwanini mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal na klabu ya west Ham nchini Uingereza Diafra Sakho aliamua kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa kilichokuwa kinashiriki katika michuano inayoendelea ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Equatorial Guinea.Sakho mwenye umri wa miaka 25 alisema alijiodoa katika kikosi cha Senegal kwa sababu ya jeraha la mgongo lakini alioneakana akichezea klabu ya West Ham na kuifungia wakati wa mchuano wa kuwania taji la FA dhidi ya Bristol City, mchuano ambao West Ham ilipata ushindi wa bao moja kwa bila, bao lililofungwa na mchezaji huyo.Sheria za FIFA zinaeleza kuwa mchezaji hawezi kuichezea klabu yake, wakati akihitajika kuichezea timu yake ya taifa.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment