Image
Image

Marekani na Korea Kusini kufanya mazoezi ya kijeshi


Korea ya Kusini na Marekani zimetangaza  kwamba zitaanza mazoezi yao ya kila mwaka ya kijeshi tarehe 2 mwezi ujao, hatua inayotazamiwa kuongeza mzozo na Korea Kaskazini.
Serikali ya Korea Kaskazini ilikuwa imeahidi kusitisha majaribio yake ya silaha za nyuklia, endapo mazoezi hayo yangefutwa mwaka huu, lakini Marekani ililikataa pendekezo hilo ikiliita “kitisho” cha kufanya jaribio la nne la nyuklia.
Mazoezi hayo ya pamoja ndicho kiini cha mzozo wa mara wa mara kwenye Rasi ya Korea, ambayo Korea Kaskazini huyachukulia kama kitendo cha uchokozi, ingawa Marekani na Korea Kusini zinadai kuwa ni mazoezi ya kujilinda.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amelitaka jeshi la nchi yake kuwa tayari kujibu “uchokozi wowote wa adui.”
Mazoezi hayo yanayojumuisha vikosi vya angani, baharini, ardhini na mtandaoni yatamalizika tarehe 24 mwezi Aprili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment