Image
Image

Rais wa indonesia Joko widodo ametaka mataifa ya kigeni kutoingilia nchi yake hata kidogo.

Rais wa Indonesia Joko Widodo amesema mataifa ya kigeni hayapaswi kuingilia haki za nchi yake kutumia sheria ya adhabu ya kifo.
Rais huyo anakabiliwa na shinikizo kutoka nchi za Australia, Brazil pamoja na Ufaransa ambazo raia wake ni miongoni mwa watu 11 wanaokabiliwa na adhabu ya kifo kwa
kusafirisha dawa za kulevya.


Hata hivyo rais Widodo amesisitiza kuwa utekelezaji wa hukumu ya kupigwa risasi hadi kufa kwa watuhumiwa hao itatekelezwa kama ilivyopangwa.
Mapema mahakama ya Jakarta ilitupilia mbali rufaa ya raia wawili wa Australia kuomba msamaha wa rais.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment