Image
Image

TPB yaunganishwa katika mkongo wa taifa wa mawasiliano


Mkurugenzi wa uendeshaji wa TPB KOLIMBA TAWA (kushoto) akipokea hati ya kukamilika kwa mradi wa Mawasilaino wa Moongo wa Taifa, (Fiber Optic), kutoka kwa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania, (TTCL), Senzige Kisenge.
Benki ya Posta nchini TPB imeunganishwa katika mkongo wa taifa wa mawasiliano wa Kampuni ya simu nchini TTCL chini ya mpango wa benki hiyo wa maboresho ya huduma za kibenki.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa TPB KOLIMBA TAWA amesema mpango huo umegharimu shilingi milioni 50 na unawezesha huduma za kibenki kuratibiwa kutoka makao mkuu ya benki ya Posta yaliyoko jijini DSM.
Naye fundi mkuu wa TEHAMA wa TTCL SENZIGE KISENGE amesema baada ya kuunganishwa katika mkongo wa taifa, benki ya POSTA itakuwa na mtandao wa internet wa uhakika na itaweza kupanua huduma za kibenki mikoani na kwa nchi jirani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment