Image
Image

Uongozi mkoani mtwara waapa kupambana na walaghai wanao didimiza wakulima wa korosho na kuwafanya kuwa Masikini.


Uongozi wa  Mkoa wa Mtwara  umesema u tapambana na wezi na walaghai wanaochangia mkulima wa kurosho kuendelea kuwa masikini licha ya kutumia nguvu na gharama kubwa katika kuzalisha zao hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara , Bibi   HALIMA DENDEGO ametoa kauli hiyo  alipokuwa   akifungua mkutano wa kazi wa wadau wa korosho unaofanyika Wilayani Masasi na kuwashirikisha wakuu wa wilaya na wakurugenzi kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi.

Amesema baadhi ya watu  wameendelea  kufaidika  na zao la korosho,   hivyo ametaka watambue kuwa Serikali ipo kwa ajili ya kusimamia haki hivyo itapambana nao kwa  g harama y o yote ,lengo likiwa kumkomboa mkulima.

Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho , Bwana  MFAUME JUMA amesema njia pekee ya kumkomboa  m kulima ni kujenga viwanda vya kubangua korosho nchini na   tayari mipango hiyo inaendelea vema.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment