Image
Image

Waziri mkuu Pinda aunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na wananchi wa kijiji cha Kmondo Mbeya

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ameunga mkono juhudi za wananchi zaidi ya 1,600 wa Kijiji cha KIMONDO katika wilaya ya MBEYA ambao wameamua kujenga Jengo la Zahanati kwa nguvu zao wenyewe, baada ya kutembea umbali mrefu wa kufuata huduma za afya.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho cha KIMONDO baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Zahanati hiyo, waziri Mkuu PINDA amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira yay sekta ya afya hasa maeneo ya Vijijini kwa lengo la kupunguza adha ya matibabu kwa wananchi.
Ujenzi wa Jengo hilo la zahanati ya kijiji cha Kimondo umeanza mwaka 2008 kwa kujitolea michango, mpaka sasa wananchi wamechangia shilingi zaidi ya Milioni 34,Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imechangia shilingi zaidi ya Milioni 7.
Waziri PINDA anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya, atakuwa wilayani Kyela ambako pamoja na kuzindua miradi ya kuboresha zao LA mpunga wa kyela, anatarajiai kukagua ujenzi wa chelezo katika bandari ya Itunge mpaka wa Tanzania na Malawi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment